
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya washiriki wa
Mkutano wa Nne wa PSPF baada ya kufangua mkutano huo kwenye ukumbi wa
Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar mjini Dodoma Februari 18, 2015.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Tuzo Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa
Rasirimaliwatu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ernest Maalugu, ikiwa
ni heshima kwa wizara hiyo kutokana na umakini wa hali ya juu katika
kuwasilisha makto ya michango ya watumishi wake kwa Mfuko wa PSPF na
utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati za watumishi wake kwa mfuko huo..
Makabidhiano hayo yalifanyika wakati Waziri Mkuu alipofungua Mkutano wa
Nne wa Mfuko wa PSPF mjini Dodoma Februari 18, 2015. Wengine kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya PSPF, George Yambesi, Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Chiku Galawa, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, na Waziri wa
Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka.(Picha na Ofisi ya Waziri MKuu).
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Fao la uzazi la Mfuko wa PSPF wakati
alipofungua mkutano wa nne wa PSPF kwenye Kituo cha Mikutano cha Saint
Gaspar mjini Dodoma Februari 18, 2015. Kulia ni Waziri wa Kazi na Ajira
Gaudencia Kabaka na watatu kulia ni Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima.
Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa, watatu kushoto
ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Maingu na wanne kushoto ni Mwenyekiti
wa Bodi ya PSPF, George Yambesi.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na watumishi wa Benki ya NMB waliokuwa
wakionyesha shughuli mbalimbali za Benki hiyo kwa washiriki wa Mkutano
wa Nne wa PSPF uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar
mjini Dodoma Februari 18, 2015.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa Nne wa PSPF wakimsikiliza Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda wakati alipofungua mkutano wao kwenye Kituo cha Mkutano
cha Saint Gaspar mjini Dodoma Februari 18, 2015.
Wasanii
wa kikundi cha Mchoya cha Dodoma wakitumbuiza katika mkutano wa Nne wa
Mfuko wa PSPF uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye kituo
cha Mikutano cha Saint Gaspar mjini Dodoma Februari 18, 2015.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiki
wa mkutano wa nne wa mfuko wa PSPF alioufungua kwenye Kituo cha Mikutno
cha Saint Gaspar mjini Dodoma Februari 18, 2015. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).








No comments:
Post a Comment